6/29/2005

Waandishi wa habari toka Kenya wafukuzwa Tanzania

Jamaa mmoja kanitumia habari hii muda sio mrefu. Imenishangaza. Soma mwenyewe.

2 Maoni Yako:

At 6/29/2005 09:05:00 PM, Anonymous maitha said...

si mara ya kwanza jambo hili kutendeka , hata mwanzoni wa mwaka kuna jamaa zangu wengine waliokuwa wameenda kufanyia ukarabati mtandao mmoja huko dar , walijikuta jela na keshoye wakarudishwa makwao

kama kweli walikiuka sheria basi sioni makosa wao kurudishwa lakini kama hawakukiuka sheria basi jambo hili huenda likaharibu misingi ambayo wanasema wananiua kuijenga kuunda jumuiya ya nchi za afrika mashariki .

labda serikali ya kenya ingeiga tendo hili pia nakuwabumburusha wote ambao wako hapa bila vibali au makaratasi maalum kwani wako wengi ambao wanaingia nchini kila kukicha na kufanya makao bila kuulizwa wametoka wapi au makaratasi yao yako wapi bora tu watoe hela basi wanageuka kuwa wakenya halisi vitambulisho na vyeti vya kuzaliwa hununuliwa bila shida .

naona nimeiteka nyara nafasi yako - wacha nihamie kwangu niendeleze jambo hili .

 
At 7/01/2005 06:31:00 AM, Blogger maka patrick mwasomola said...

Hapa tuache sheria ichukue mkondo wake tusiharibu utaratibu kwa kisingizio cha jumuia ya Afrika ya Mashariki ndo maana wale jamaa waliokwapua pesa katika mabenki yetu sheria ilichukua mkondo wake na alio hatiani walitiwa hatiani na wasio na hatia waliachiwa huru sasa je wangeachiwa kwa kisingizio tu cha jumuia kuvurugwa?Hata kama Kenya na Uganda kuna watanzania wanavunja sheria kwa kisingizio cha jumuia nao pia washughulikiwe bila kuonewa.
Tujenge jumuia huru na ya haki yenye kufuata misingi yote ya sheria bila kujali kuwa huyu ni wa wapi sidhani kama serikali zingine yaani kenya na uganda mtanzania akifanya makosa basi watasema tunaacha kwa ajli ya kivuli cha jumuia.UHURU!

 

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com