6/21/2005

NINAKWENDA KUBLOGU MKUTANO WA G8

Waandishi saba wa Afrika, nikiwemo kati yao, tutakwenda Uingereza, pamoja na mambo mengine, kuhudhuria mkutano wa G8 utakaofanyika tarehe 6-8 mwezi ujao kule Uskochi. Safari yetu itakuwa ya wiki mbili (wiki moja katika jiji la London na wiki nyingine Edinburgh. Tutakuwa katika mpango uitwao G8 Media Fellowship wa shirika lisilo la kiserikali la Panos London. Waandishi wengine watakaoshiriki wametoka Kenya, Uganda, Malawi, Sierra Leone, na Msumbiji. Moja ya madhumuni ya mpango huu ni kuwawezesha waandishi wa habari toka Afrika kuweza kuwa na ufahamu zaidi juu ya masuala ya sera na mikutano ya kimataifa. Pia itawawezesha kuandika habari kuhusu mkutano huo kupitia mtazamo wa Waafrika wenyewe.
Tembelea shirika la
Panos kujua zaidi juu ya kazi zake.

*******************************************************************************

Maombi yangu ya visa ya kwenda Uingereza yamekubaliwa leo. Hivyo nitaondoka jumapili kwenda huko kwa Malikia Lizabeta. Nikiwa huko nitablogu hapa Jikomboe juu ya mkutano na matukio mengine yanayohusiana na mkutano wa nchi nane za kibepari. Pia shirika la Panos linatengeneza blogu maalum kwa ajili ya mkutano huo. Nikishapata anuani ya blogu hiyo nitaweka hapa.

Nikiwa ninablogu kwa Kiswahili kupitia Jikomboe,
Mshairi, mwanablogu toka Kenya anayeishi Uingereza amenieleza kuwa ana nia ya kutafsiri (nitakayokuwa naandika kwa Kiswahili) kwa kiingereza kwenye blogu yake. Namshukuru kwa uamuzi wake huo wa kujitolea.

5 Maoni Yako:

At 6/22/2005 08:16:00 AM, Anonymous mshairi said...

Hongera, Ndesanjo.

And thanks for the mention.

 
At 6/22/2005 01:53:00 PM, Anonymous mwana nchi said...

Yaani na kelele zako zote za kuwashutumu akina kichaka na mapebari unakwenda kwenye mkutano wao? Hapo umetuangusha!

 
At 6/22/2005 11:49:00 PM, Anonymous mkulima said...

mwana nchi kasema kweli. Kwanini usiblogu vikao vya wakulima na wafanyakazi unaenda kublogu mkutano wa mabepari? Unatuhusu nini?

 
At 6/23/2005 02:34:00 AM, Blogger Mija Shija Sayi said...

Ukitaka kummaliza mbaya wako ni lazima umjue kiundani, kwenda kwa ndesanjo katika mkutano wa mapebari haimaanishi anawaunga mkono...la hasha, ni katika kutaka kupata habari zaidi. Tukumbuke mabepari hawa hawa wasiotupenda hujidai wanatupenda kwa kuja kwetu na kujishirikisha na shughuli zote za kijamii ili tuwaone watu wazuri, lakini lao hasa liko moyoni, ni kutaka kutujua kiundani ili wajue watumalizeje. Kwa hiyo tusiwe na wasiwasi kwa bwana Ndesanjo kwenda mkutanoni hana nia mbaya.

 
At 6/23/2005 01:05:00 PM, Anonymous Mtoto wa Nyerere said...

Ndesanjo, hivi hadi leo huwajui hawa mabepari na nia yao? Toka zamani nia yao ni ile ile haijabadilika. Nini zaidi unataka kujua kuusu wao?

 

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com