6/17/2005

SKOLASHIPU KWA WANABLOGU/WAANDISHI AFRIKA

Mkutano uitwao Highway Africa wa mwaka huu unafanyika Septemba huko Grahamstown, Afrika Kusini. Kuna nafasi chache za skolashipu kwa waandishi walioko Afrika. Nadhani wanablogu walioko barani wanaweza kuomba nafasi hizo hasa kutokana na ukweli kwamba katika mkutano huo kuna msisitizo wa matumizi ya zana mpya za mawasiliano na habari. Mwisho wa kuomba ni tarehe 7 mwezi ujao. Nenda hapa kwa taarifa kamili za mkutano na maelezo jinsi ya kuomba. Wanasisitiza kuwa ukiomba lazima UWE MWANDISHI WA HABARI.

2 Maoni Yako:

At 6/18/2005 03:36:00 AM, Anonymous Anonymous said...

Asante macha kwa taarifa.

 
At 6/19/2005 09:07:00 AM, Anonymous Anonymous said...

Taarifa kama hizi muhimu kutoa kwenye vyombo vya habari. Watu wengi huwa wanasikia siku zikiwa zimeshapita.

 

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com