9/15/2004

KWA TAARIFA YAKO...

Kwa taarifa yako...
Hakuna kitabu chochote katika Biblia ambacho kimeandikwa na nabii Musa. Kanisa lilinidanganya kwa miaka mingi sana nikadhani kuwa ni kweli vitabu hivi viliandikwa na Musa. Musa hakuandika kitabu hata kimoja.

Kama vitabu vitano vya mwanzo vya Biblia vimeandikwa na Musa kwanini aandike, "...Mungu akamwambia Musa..." badala ya kuandika "Mungu akaniambia..." Mtu akikwambia jambo huwa hatusemi, "Fulani akamwambia..." bali tunasema, "Fulani aliniambia..."

Na iweje Musa aandike hadi kifo chake mwenyewe? Kitabu cha Kumbukumbu la Torati: 34:7 kinasema: Musa alikufa akiwa na miaka 120...
Inawezekana mstari huu Musa aliuandika kabala hajafa! Au aliuandika kimiujiza baada ya kufa?

Uongo mwingine ni kuwa vitabu vya Injili ya Matayo, Marko, na Luka vimeandikwa na wanafunzi wa Yesu. Hawa mabwana hawakuwa wanafunzi wa Yesu. Yote waliyoandika waliandika kutokana na mambo waliyoyasikia toka kwa wale waliomuona Yesu! Tatizo ni kuwa hata mahakamani ushahidi wa mambo uliyosikia (hearsay) hauna nguvu!

0 Maoni Yako:

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com