9/15/2004

MABANGO YA KISIASA NJE YA NYUMBA

Jumba la nne mtaa wa Robinwood, karibu na makutano ya Robinwood na Bancroft ni uwanja wa siasa. Nje ya jumba hilo kuna bendera ya Marekani na ya Umoja wa Mataifa zinapepea. Kitendo cha kuweka bendera ya Umoja wa Mataifa kinanifanya nitambue kuwa mwenye jumba hili lilojengwa miaka mingi iliyopita ni mtu wa siasa za mrengo wa kushoto. Watu wenye siasa za mrengo wa kulia wanauponda sana Umoja wa Mataifa. Hawaoni sababu ya maana ya MArekani kuwa mwanachama wa Umoja huu. Wananchi wa siasa za kushoto kama huyu bwana wanaona kuwa umoja huu pamoja na matatizo yake mengu bado una manufaa kwa taifa na dunia kwa ujumla.

Jana jioni nikiwa narudi toka mizungukoni na rafiki yangu Malaika jamaa alikuwa nje ya nyumba yake akiwa amemaliza kuweka mabango matatu meupe yaliyoandikwa kwa rangi nyekundu. Yameandikwa hivi kwa herufi kubwa:
WAIRAKI WALIOKUFA: 12, 721
WAMAREKANI WALIOKUFA: 1, 014
WAMAREKANI WALIOJERUHIWA: 7, 032

Hizi ni takwimu zinazotokana na uvamizi wa kigaidi wa Marekani dhidi ya Iraki. Kila siku atakuwa anabadili takwimu hizi kuendana na yanayotokea huko Iraki.

Hii tabia ya watu wa mtaa huu wa Old West End kuweka mabango ya kisiasa nje ya nyumba zao unanifurahisha sana. Nitapiga picha baadhi ya mabango haya na kuweka ndani ya blogu hii.

0 Maoni Yako:

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com