9/10/2004

JABALI AFRIKA (Sisi Tambala wa Kenya)

Kila ninapowasikiliza hawa jamaa wa Kenya wanaojiita Jabali Afrika ninakumbuka sana kundi la Sisi Tambala (bado wanafanya mazoezi pale nyumba ya sanaa?). Jabali Afrika wanaimba kiafrika na kupiga ngoma. Niliwasikia mara ya kwanza mwaka 2001 niliponunua kanda yao pale Nairoberry (Nairobi) nikitokea Kisumu. Ilikuwa ni kanda ya CD yao iitwayo Journey. CD yao ya mwisho kutoa, Rootsganza sijaipenda sana. Naona wameingiza vyombo kadhaa ambavyo vimeharibu kabisa ule utamu wa sauti zao na midundo ambayo inanikumbusha sana afrika. Ila Maumau Chant katika CD hiyo ni kiboko. Hatari tupu. Mshairi Cosmas Sindani (ninatafuta habri zake zaidi) ndio hasa amenikuna. Huku ngoma zikirindima kwa mtindo wa Nyanbinghi, Sindani anaghani kwa sauti iliyojaa hisia, "Mzungu arudi Ulaya, Mwafrika apate Tawala." Ninapanga kwenda Cleveland mwezi huu kwenye shoo yao. Tazama picha zao kwa kubonyeza hapa.

0 Maoni Yako:

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com