UNAFAHAMU TOVUTI HII YA VIJANA TANZANIA?
Hawa jamaa siwafahamu vizuri. Ndio kwanza nasikia harakati zao. Tazama tovuti yao hapa. Nitatafuta habari zaidi juu ya juhudi zao za kukomboa vijana wa Tanzania waliosahaulika na mfumo wa utawala. Pia nitapenda kuwasiliana nao juu ya lugha. Hili tatizo sijui litaisha lini. Wanatengeneza shirika na tovuti inayohusu vijana walalanjaa wa Tanzania kisha wanaandika mambo humo ndani kwa lugha ambayo hawaitumii? Kama wanatetea vijana wa Uingereza tutawasamehe. Ila kama wanaongea na vijana wa Tanzania ambao kwa masaa 24 lugha yao ni Kiswahili, lakini kwasababu tusizoelewa wanatumia kiingereza (tena chenye mabomba kebekebe), tutawauliza. Tutawaandama. Hii vita sijui nani atajiunga nami. Vita ya kusafisha mashirika yasiyo ya kisirikali, wasomi, sirikali, bunge, mahakama, n.k. na kasumba ya kukimbilia lugha ambayo asilimia kubwa ya Watanzania hawaijui na hata wanaoijua hawaitumii katika shughuli zao za kila siku. Niliwahi kuzungumzia juu ya majina ya kiingereza ya mashirika haya, majina ya kiingereza ya vyama vya siasa, kiingereza kwenye tovuti za bunge na ikulu, n.k. Wakati huo huo utasikia watu wakisema kuwa lugha yetu ya taifa ni kiswahili. Kama haya mashirika, vyama, tovuti, n.k vimeanzishwa kwa ajili ya watu wanaoitwa eti "wafadhili" ambao kawaida ni watu weupe, WATUAMBIE. Watanzania hatutaki kutaniwa!
0 Maoni Yako:
Post a Comment
<< Home