2/01/2005

TAMASHA LA BOB MARLEY

Kuna tamasha kubwa la Robert Nesta Marley (Bob Marley au Bobu Malya) kule Ethiopia. Tamasha hili ni la kumbukumbu ya miaka 60 toka kuzaliwa kwake. Kati ya wanaotazamiwa kutumbuiza huko ni mama yake Bob, Cedella Booker, mke wake, Rita Marley, na watoto wake watano, Angelique Kidjo, Indie Arie, Youssou Ndour, na wengineo. Tamasha hili limeitwa Africa Unite kutokana na wimbo alioimba Bob Marley akilitaka bara la Afrika kuungana kwa kuwa itakuwa ni "jambo jema mbele ya mungu na mwanadamu kuona Afrika imeungana." Nitaandika zaidi juu ya tamasha hili na mengine kuhusu Bob Marley. Mengi zaidi ni leo jioni. Kwa sasa nenda hapa.

0 Maoni Yako:

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com