2/05/2005

MJI MKUU WA TANZANIA NI...

Usiniulize swali hili. Wakati nikiwa shuleni nilikuwa nikijibu kwenye mitihani kuwa mji mkuu wa Tanzania ni Dodoma. Walimu walikuwa wanatudanganya hivi hivi tukiona. Hakuna jambo baya kama kupitia mfumo wa elimu ambao unafundisha uongo uliochanganywa na vipande vidogo vidogo vya ukweli. Eti mji mkuu wa Tanzania ni Dodoma! Nasikia hadi leo wanafundisha uongo huu mashuleni.
Mwanablogu wa Blogu ya Mavituvitu ndio kanikumbusha hii habari ya mji mkuu. Hivi sasa anablogu toka bungeni Dodoma. Mfuatilie. Anasema kuwa kati ya miswada wanayopitia ni huu hapa.

0 Maoni Yako:

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com