9/18/2004

NIJIITE X???

Ninaanza kuchoka kumfunza kila ninayekutana naye jinsi ya kutamka jina langu: ndesanjo. Wengine wanasema, "Basi nitakuita Macha." Lakini nawaambia kuwa Macha ni jina la familia/ukoo. Macha sio jina langu. Mimi ni Ndesanjo! N'takuzaba kibao mimi...

Wengine wanapata tabu kulitamka kiasi ambacho utadhani kuwa wanaweza kuvunja jino! Tuache utani, ninaanza kukerwa. Sina muda wa kufundisha kila ninayekutana naye. Ninakutana na watu kibao kila siku. Kuna mambo mawili naweza kufanya: nianze kutoza kodi (si ndio ubepari wenyewe huu?) kila ninapofundisha mtu au nikate mzizi wa fitina na kufuata nyayo za Malcolm X kwa kujiita X!

0 Maoni Yako:

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com