7/28/2004

UNYAMA, UNYAMA...MUNGU MKUBWA!

Jina la Mungu limetumiwa miaka nenda rudi kuhalalisha unyama. Mwizi wa kura George Bush na wahafidhina wenzake wanadai kuwa vita wanavyoviongoza dhidi ya "ugaidi" ni vita ya wenye Mungu wa kweli dhidi ya wafuasi wa shetani. Makundi yanayojiita kuwa ni ya kiislamu nayo yanafanya unyama dhidi ya wengi wasio na hatia kwa madai kuwa wanapigana vita vya kidini. Wanampigania Mungu wa kweli! Mwanazuoni mmoja, jina limenitoka, aliwahi kusema kuwa dunia ina dini za kutosha kutufanya tuuane, tugombane, na kuchukiana lakini hakuna dini za kutufanya tuishi kama ndugu.

Tazama picha hii ya unyama usio na mfano uliofanya dhidi ya Mmarekani Nick Berg. Napenda kukutaarifu kuwa picha hii, hasa mwishoni, inatisha na kuchafua roho kabisa. Kama una roho nyepesi nakushauri usiitazame. Kongoli hapa uione.


1 Maoni Yako:

At 7/29/2004 01:01:00 PM, Blogger maka patrick mwasomola said...

Ndesanjo,binadamu ni wanyama.Hatuna utu hata kidogo.Ninajua kuna watu wengi sana wanakufa kinyama huko Iraqi,Palestine na kwingineko duniani.Lakini unajua mabeberu hawatuonyeshi picha kama ya masikini kijana Nick Berg.
Kwa kweli nimesikitika sana,na imeniuma sana.Nimeshindwa kutazama zile picha za mwishoni,machozi yamenitoka Ndesanjo,siwapendi Bush na utawala wake kutokana na sera zao,lakini ninampenda nitamuenzi,nitamuheshimu masikini Berg.Amekufa bila hatia huyu kijana amekufa kishahidi yeye na wengine wote waliouawa kama yeye.Ninaweza kusema tu yeye ni muathirika wa sera za rais kichaka.Yeye,pamoja na wananchi wote wa Iraqi waliopoteza maisha kwa njia moja au nyingine kutokana na unyama wa Marekani wapumzike kwa amani.
Berg jamani sisi wanadamu lazima tutambue kuwa amekufa kwa uchungu sana amekufa anajiona.Nilimuangalia sana Ndesanjo,nikawaangalia wale jamaa,jinsi walivyochomoa jambia jinsi walivyomkata.Mwenyezi Mungu utusamehe sisi waja wako ninafikiri kuwa hatujui tulifanyalo.Ni mapambano ambayo sisi wote kama binadamu tayari tumepoteza.Tunapambana kwa ajili ya nini?
Ni kweli kuwa kuna dini nyingi sana humu duniani za kutufanya tuuane,tuchinjane tutupiane makombora mazitomazito,tusiaminiane,lakini hakuna kamwe dini ya kutufanya tuishi pamoja,hakuna.Berg,na wengine wa aina yake wametufundisha kuwa kamwe hakuna dini ya namna hiyo.Na Ndesanjo sijui kama itakuja kuwepo dini ya namna hiyo.
Ninafikiri Bush lazima atakuwa ana matatizo lakini sisi kutokana na kuwa yeye ana nguvu basi hatulioni hilo.
Hivi kwani Berg hakuwa na wazazi?Ninamaana kuwa watoto wa Bush na watoto wa viongozi wengine watajisikiaje kuona baba zao wamekubali mtoto wa mwenzao auawe kama kuku? Hawana uchungu?Hawana uchungu kweli na Berg.
Berg amekufa kijasiri sana.Unajua Ndesanjo wakati ninaangalia video ile nililiona lile tukio kama ni live.Nilimuangalia sana yule kijana,sura yake ilikuwa inazungumza kitu fulani lakini sijui ni kitu gani,sawa alikuw muoga lakini ukiangalia sana alikuwa na ujasiri wa hali ya juu sana.Aliamua kupokea chochote kitakachotokea.
Sasa basi ninakili waziwazi kuwa mama Aroyo na waziri mkuu wa Hispania ni watu wenye akili sana na busara sana kuliko rais Bush.Thamanai ya maisha ya binadamu huwezi kuilinganisha na kitu chochote kile hapa duniani,ndiyo mana yule mama na yule bwana wa Kihispaniola walilijua hilo mapema.Mungu awabariki sana hawa watu.Nimesikitika,kuhuzunika na kusonononeka na suala zima la masikiniBerg.Peace may prevail in this world.

 

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com