6/20/2004

Ubepari ndio tunaoutaka?

Mfumo wa uchumi wa kibepari ni kama barabara ya lami mchana wa jua kali. Ukiwa barabarani unaona mbele yako kama vile kuna maji. Kiingereza wanasema hiyo ni mirage. Ndivyo ilivyo hili taifa. Umasikini, hujuma, rushwa, magonjwa ya akili, ukimwi na vitu kama hivyo vimefichika sana. Je unajua kuwa watu milioni 43 hawana bima ya afya? Kama huna bima ya afya katika nchi kama hii wewe ni kama binadamu asiye na uhai!

Ninatazama sinema iitwayo Waco. Unakumbuka lile kundi la dini na Branch Davidians ambalo mwanzo wa miaka ya 1990 lilikuwa na ugomvi na serikali kisha yakatokea mapigano na FBI. Jumba lao liliungua moto. Serikali ilidai kuwa waumini hao waliamua kujiua. Wengine wanadai kuwa serikali iliwaua. Sinema hii inachambua kwa kina tukio hili. Habari zaidi za Branch Davidians nenda hapa

1 Maoni Yako:

At 6/27/2004 02:46:00 PM, Anonymous Anonymous said...

Hawa wananikumbusha stori ya Kibwetere kule Uganda na Jim Jones kule Guyana nadhani mwaka 1974. Kibwetere sikumbuki vizuri ila sio miaka mingi iliyopita.

 

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com