3/04/2005

UTAJUAJE KAMA UKO MTAA WA MASIKINI NCHINI MAREKANI?

Juzi niliandika mambo kadhaa ambayo yanakujulisha kuwa uko mitaa ya walalanjaa hapa Marekani. Rafiki yangu kanikumbusha jambo moja muhimu sana nilisahau. Ninarudia kuandika niliyokuwa nimeandika awali na kuongeza moja alilonipasia rafiki wangu huyu:

Swali: Unawezaje kujua kama mtaa fulani ni mtaa wa watu masikini nchini Marekani?

Jibu: Utajua kuwa mtaa ni wa masikini pale utakapoona vitu hivi:

1. Makanisa kila kona

2. Msururu wa maduka yanayouza pombe na tiketi za bahati nasibu

3. Magari ya polisi kila kona na ving'ora kila dakika

4. Magari yenye muziki uliofunguliwa kwa sauti ya juu kabisa

5. Watu wenye mapengo wakati bado hawajazeeka! (hii ndio kanikumbusha rafiki yangu).

0 Maoni Yako:

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com