UKWELI KUHUSU KARUGENDO NA KANISA KATOLIKI
Hayawi hayawi...
Leo ninakupa barua aliyoandika Padri mpenda mabadiliko, Padri Privatus Karugendo, kwa Askofu Methodius Kilaini wa jimbo la Dar Es Salaam. Kanisa Katoliki limemsimamisha kazi ya Upadri, Padri Privatus Karugendo. Katika barua hii tutapata ukweli juu ya mgogoro kati ya kanisa na Padri Karugendo. Utaona kuwa moja ya hasira za kanisa (linalofundisha kusamehe mara saba u sabini) dhidi ya Padri Karugendo ni kitendo chake cha kusoma kitabu kinachotoa changamoto kwa waumini wa Kikristo kiitwacho JESUS THE MAN kilichoandikwa na mtafiti na mwana teolojia Barbara Thiering. Kitabu hiki, pamoja na mambo mengine, kinaonyesha kuwa Yesu hakuzaliwa kwa uweza wa roho mtakatifu kama kanisa linavyodai, na pia alimuoa Maria Magdalena na baadaye kuachana naye na kisha kumuoa Lidia. Mwandishi huyu ana kitabu kingine kiitwacho The Book That Jesus Wrote.
Sasa soma barua ya Padri Karugendo kwa kubonyeza hapa. Kumbuka kuwa makala zake nyingine ziko katika kona yake iitwayo Kalamu ya Padri Karugendo iliyoko upande wa kuume, shuka chini ya picha yangu, makala zangu na za Freddy Macha, utakuta safu yake. Kesho nitapandisha makala nyingine. Pia tarajia kupata undani zaidi wa chuki ya kanisa Katoliki dhidi ya watumishi wanafumbua macho na kutaka mabadiliko ya mfumo huu wa imani uliojengwa katika misingi ya mfumo dume na kujaa sheria za wanadamu wanazodai kuwa ni za mungu.
0 Maoni Yako:
Post a Comment
<< Home