3/01/2005

KESI YA AINA YAKE MAREKANI

Kuna kesi ninayoifuatilia kwa karibu ambayo imechukua sura mpya. Kwanza ilikuwa ni ugomvi kati ya mume na wazazi wa mke wa jamaa. Mke wake ni mgonjwa asiyeweza kuongea wala kufanya lolote kwa miaka 15. Mume kaenda mahakamani kuomba aruhusiwe kuchomoa mrija wa kumlishia chakula ili afariki. Mume anadai kuwa hayo ni mapenzi ya mke wake. Hapendi kuishi katika mateso. Alimwambia wakati akiwa mzima. Wazazi wa mke wanadai kuwa mtoto wao ana haki ya kuishi na anaweza kupona. Mahakama ilikubali ombi la mume.

Sasa wazazi wa binti wamekuja na mpya: wanaomba talaka kwa niaba ya binti yao dhidi ya mue wake, ambaye wanadai ana watoto na mwanamke mwingine anayeishi naye hivi sasa. Hivi kwanini ninapoteza muda badala ya kukwambia ubonyeze hapa?

0 Maoni Yako:

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com