3/04/2005

KANISA KATOLIKI NA PADRI KARUGENDO

Kanisa lenye "demokrasia" ya kuoongozwa na wanaume tu (na Mapapa toka Uropa) limekuwa likimwandama Padri Karugendo kupitia gazeti lake la KIONGOZI. Askofu Severini Niwemugizi wa jimbo la Katoliki la Rulenge aliandika barua kwenye gazeti hilo akidai kuwa Padri Karugendo amemkashifu. Padri Karugendo akaandika barua ya majibu na kutuma kwa mhariri wa gazeti hilo. Barua haikutolewa. Hii sio ajabu kwa watu wenye kujua historia ya kanisa hili. Sasa barua ya Padri Karugendo nimeianika hapa bloguni muisome. Na kama Askofu Niwemugizi (ninapaswa kumwita "Baba" Askofu???) anataka kuijibu, anaruhusiwa kuijibu. Blogu hii haitakataa kuitoa kama gazeti la kanisa lake lilivyofanya. Bonyeza hapa uisome. Kumbuka makala zake nyingine ziko katika safu yake iitwayo Kalamu ya Padri Karugendo iliyoko hapa ndani ya blogu, mkono wa kuume, shuka chini ya makala zangu na za Freddy Macha utakumbana na safu yake. Padri Karugendo ana safu pia kwenye gazeti la kila alhamisi nchini Tanzania liitwalo Rai (nguvu ya hoja).

0 Maoni Yako:

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com