3/28/2005

Kwanini haiwezekani?
Wananiambia kuwa haiwezekani. Kwanini?
Eti wananiambia kuwa haiwezekani ukawa hauko CCM na ukawa hauko upande wa upinzani.
Haiwezekani. Lazima uwe na upande. Lazima uwe kushoto au kulia. Ukiikosoa CCM wanakuja juu na kusema, "Wewe unashabikia upinzani." Ukikosoa upinzani wanakuja juu, "Umetumwa na CCM." Ukikosoa upinzani na CCM kwa pamoja wabaki mdomo wazi. Wanasema, "Haiwezekani!"

Jambo gani gumu kuelewa? Nawauliza.
Kwani ni kosa kutokuwa upande wowote? Naendelea kuwauliza.

Wananiambia lazima nichague shetani mwenye afadhali. Lazima nitafute mwivi na muongo mwenye afadhali. Lazima nichague shetani mmoja kati ya wawili.
Kwanini kuwe na ulazima huo? Naendelea kuuliza.

Mimi sitaki shetani wa upande wa kuume wala shetani wa upande wa kushoto. Awe ni shetani mwenye afadhali au shetani asiyefaa kabisa. Sitaki muongo au mwivi bora zaidi ya mwingine.


Inawezekana.

0 Maoni Yako:

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com