2/05/2005

RAIS MWENYE REKODI YA KUKAA MADARAKANI AFARIKI

Rais wa Togo, Gnassingbe Eyadema, ambaye ndiye kiongozi aliyekaa madarakani kwa muda mrefu kuliko wote Afrika, amefariki dunia. Eyadema amekalia kiti cha urais toka alipofanya mapinduzi ya kwanza Afrika (baada ya ukoloni) mwaka 1967.

Unaweza kuamini? Jamaa kawa Rais toka 1967! Watu wanazaliwa na kuanza kuzeeka wakimsikia rais huyo huyo. Afrika safari ya demokrasia bado ni ndefu. Ingawa katiba ya Togo inatamka kuwa atakayechukua madaraka iwapo rais ataaga dunia ni spika wa bunge, mtoto wa Eyadema ndiye aliyetawazwa kuwa rais. Sijui kwanini wasiseme kuwa Togo ni nchi ya kifalme. Urais unarithiwa kama shati.

Ukiacha Fidel Castro wa Cuba ambaye amekuwa madarakani toka 1959, hakuna kiongozi mwingine duniani anayemtoa Eyadema katika mchuano wa kukalia kiti cha urais kama vile amezaliwa nacho.

Niliwahi kusema zamani kidogo katika moja ya makala zangu kuwa, kuna uwezekano mkubwa tukaanza kusikia vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Togo baada ya Eyadema kufariki. Bado nina hisia hizi.

0 Maoni Yako:

Post a Comment

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com