9/28/2004

DARFUR YA MAREKANI

Wamarekani wanapenda sana kuuliza kwanini Waafrika wanauana katika vita kama vile hawana akili timamu? Wakati ambapo hapa Marekani hakuna mauaji ya halaiki (ya wazi wazi!!!) kama kule Sudan au Rwanda, kuna mauaji baina ya mtu na mtu yanayonifanya nitishike sana ninapoona mtu ananijia akiwa na mkono mfukoni. Bonyeza hapa usome kisa hiki kilichotokea jana huko Detroit. Visa kama hivi vinatokea kila kukicha. Jamaa anaweza kuwa ameudhiwa na mke wake anaamua mguu na njia na bunduki yake kutafuta watu wa kuwamwagia risasi.

0 Maoni Yako:

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com