5/30/2005

UNAWEZA KUTAZAMA VIDEO KWA MIAKA 68?

Paula LeDieu, aliyewahi kuwa mkurugenzi wa idara ya nyaraka huru za shirika la habari la BBC, aliongea jioni ya tarehe 26 katika mkutano wa Commons-Sense. Alitumia kama dakika ishirini hivi kuzungumzia uamuzi wa shirika hilo kutumia modeli ya hatimiliki ya Creative Commons. Mradi uitwao The Creative Archive unaruhusu wakazi wa Uingereza (kwakuwa kodi yao ndio inaendesha shirika hili) kutumia kwa njia zozote zile (isipokuwa kibiashara) nyaraka zote za shirika hilo. Mradi huu ulianza rasmi mwaka jana.

Kwakuwa BBC ilianzishwa mwaka 1922, rundo la nyaraka ambazo imehifadhi ni kubwa kiasi ambacho inakupasa ukae mbele ya luninga yako ukitazama bila kuzima kwa miaka 68, masaa 24 kwa siku! Utaweza?

1 Maoni Yako:

At 6/03/2005 02:32:00 AM, Blogger Rama Msangi said...

Ikiwa umri wetu wa kuishi tu hauwezi kufikia kiwango hicho, hakika ni vigumu sana kwa jambo kama hilo kutokea. Utajifunza kusoma lini na uje ufikie muda wa kutizama hiyo video kwa muda huo?, hakika itakuwa miujiza.

 

Post a Comment

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com