4/20/2005

UNAMFAHAMU ETHAN ZUCKERMAN

Juzi jumapili nilikutana na mmoja wa watu ambao nimekuwa nikiwafuatilia kwa muda mrefu toka nianze kujiingiza katika masuala ya blogu na teknolojia mpya za mawasiliano na habari, Ethan Zuckerman. Tulikutana katika mgahawa huu hapa. Tulizungumza juu ya mambo mbalimbali kuhusu blogu za Kiswahili na mradi anaoendesha wa Global Voices. Ni siku nyingi sana toka nikutane ana kwa ana na mtu anayeelewa kwa undani masuala ya teknolojia na pia siasa na tamaduni za Afrika na nchi nyingine duniani.
Nitaongelea kwa undani mazungumzo yetu baadaye. Kwa sasa ningependa umfahamu Zuckerman. Ethan Zuckerman ni mtafiti katika chuo kikuu cha Harvard. Habari zaidi juu yake hapo Harvard na mengine ambayo amewahi kufanya hapa. Soma blogu yake hapa. Pia kuna mahojiano yake hapa. Anajihusisha na mradi wa world changing. Kongoli hapa. Na mkono wake uko nyuma ya mradi huu hapa.0 Maoni Yako:

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com