DINI WALIZOANZISHA WAAFRIKA UTUMWANI
Ingawa Wafrika waliofika utumwani ughaibuni walikatazwa kuwa na imani zao za asili, Waafrika wengi walitumia mbinu ya kuchanganya kitu kinachoitwa ukristo (baadaye nitaeleza kwanini ninasema, "kitu kinachoitwa ukristo.") na imani zao za asili. Walitumia pia nyimbo za kanisani kupeana habari za siri kama vile mipango ya kutoroka, mikutano ya siri, njama za kuvamia "mabwana" utumwa, n.k. Katika dini ambazo ziko hai hadi leo zinazotokana na harakati hizi za Waafrika kutunza imani zao za asili na kukabiliana na mazingira mapya ambayo yalikataza imani hizo ni candomble na umbanda huko Brazili, Vodun huko Haiti na Marekani, Santeria huko Cuba na Puerto Rico, na shango huko Grenada, Trinidad na Tobago.
0 Maoni Yako:
Post a Comment
<< Home