8/22/2004

NIMERUDI

Ndio ndugu zanguni,
Nimerudi usiku wa leo. Nina rundo la barua pepe toka kwenu ambazo zitaweza kuzipitia na kujibu. Ninahitaji kupumzika. Ninashukuru walioniandikia. Walioniuliza maswali nitawajibu.

Ndugu Maka Patrick Mwasomola ninashukuru kwa kunikumbusha juu ya Siti Binti Saad (1880-1950). Nitaandika kidogo juu ya mwanamama huyu ambaye watu wanataka kumsahau ila historia inakataa.

Mwasomola katuma ubeti toka Diwani ya Shaban Robert, Siti Binti Saad, Kitabu cha Tatu:
Siti Binti Saad,ulikuwa mtu lini?
Ulitoka shamba,
na kaniki mbili chini
Kama si sauti ungekula nini?

Ninapumzika kisha nitarudi. Safari imenichosha. Nina mambo kadhaa mapya. Kaa chonjo!

4 Maoni Yako:

At 8/24/2004 09:51:00 AM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Huyu mama alisafiri hadi India kuimba zamani hizo. Sisi sema hatujali watu wetu.

 
At 8/24/2004 09:51:00 AM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Sitti alikuwa kinara wa muziki kanda ya bahari ya nhindi

 
At 8/24/2004 09:53:00 AM, Blogger Ndesanjo Macha said...

kuna hadithi mbili hujamalizia bado.

 
At 8/26/2004 09:33:00 AM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Huwezi kuzungumzia taarab bila kumzungumzia huyu mama.

 

Post a Comment

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com