8/14/2004

Makala Mpya

Nimeweka makala mpya. Tazama mkono wa kuume, peleka kiteuzi, kongoli, kisha isome. Ni makala mpya hapa kwenye blogu yangu ila ilitolewa kwenye gazeti la Mwananchi zamani kidogo. Jumapili hii katika ukurasa wangu gazeti la Mwananchi ninaongelea masuala ya utamaduni, lugha za asili, na Ngugi wa Thiong'o. Makala inaitwa: Je mnamtabua Shetani Msalabani? Kicha hiki kinatokana na jina la kitabu cha Ngugi alichoandika kwenye karatasi za chooni akiwa jela kwa lugha ya Gikuyu kiitwacho Caitaani Mutharabaini (Shetani Msalabani). Nitaiweka makala hiyo hapa ndani jumapili jioni au jumatatu.

2 Maoni Yako:

At 8/15/2004 05:11:00 AM, Blogger maka patrick mwasomola said...

Nimesoma leo katika gazeti la mwananchi, inatukumbusha shuleni,Ngugi ni mtunzi mahili huwa sichoki kumsoma na ninavyo vitabu vyake karibia vyote.Lakini sijawahi kusoma kitabu chake cha homecoming,na Decolonising the mind ninafikiri ni vizuri sana.Lakini mashetani walioko msalabani hivi majuzi walimvamia na kumpiga na kumuibia yeye na mke wake nyumbani kwao Nairobi.

 
At 8/15/2004 11:23:00 PM, Anonymous Anonymous said...

Nafuu tuweze kusoma makala zako. Hogera usichoke.

 

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com