Mwandishi wa Kenya akataliwa kibali Tanzania
Je uamuzi wa serikali unaweza kuchukuliwa vipi katika mazingira ya Jumuiya ya Afrika Mashariki? Soma kisa chenyewe hapa.
BLOGU YA KISWAHILI KWA AJILI YA KUSAFISHA FIKRA ZA WAAFRIKA!
Je uamuzi wa serikali unaweza kuchukuliwa vipi katika mazingira ya Jumuiya ya Afrika Mashariki? Soma kisa chenyewe hapa.
posted by Ndesanjo Macha @ 8/16/2005 04:28:00 PM 3 comments
You can also find me @: Jikomboe(Kiswahili)
Mwongozo (A Blogging Guide In Swahili)
Global Voices Online
3 Maoni Yako:
Uamuzi uliochukuliwa na serikali dhidi ya watu kama Waweru unaweza kuwa wa kushtua na kufurahisha wakati huo huo.Itategemea unaliangalia suala hili kwa mtizamo gani na upo katika kundi gani la kiutendaji.
Unaweza kuwa wa kufurahisha kwa watanzania ambao wana sifa za kitaaluma na uzoefu pengine hata kuzidi alizonazo Waweru lakini hawana kazi.Hili limetokea sana tu katika nchi kama Tanzania jambo ambalo linazidi kusababisha "drain brain" kwa nchi zetu.Ajira zinazowafaa wananchi zinaenda kwa wageni.Matokeo yake ni wasomi wengi kutimkia Ulaya na Marekani.Kama kuna watanzania wenye sifa za kutosha kuwa CEOs nk kwanini ajira isiwe yao? Nini faida ya uwekezaji basi wakati hata faida yote inaenda nje ya mipaka yetu?Ajira kwa wananchi ni muhimu sana katika kuonyesha matokeo bora ya wawekezaji.
Uamuzi huo huo sio wa kufurahisha kwa wengine ambao nia na madhumuni yao ni kuwekeza ili kuongeza ajira na sio kuwanyang'anya ajira na maliasili zilizopo(investors).
Ubaya wa tukio kama hili lililomkumba Waweru ni Tanzania kupewa kisogo na wawekezaji wengine. Mara nyingi wawekezaji hawataki kubughudhiwa na kufuatwafuatwa juu ya masuala yao ya kiuongozi.Ni vyema serikali ya Tanzania ikawa wazi wakati wawekezaji hao wanakuja nchini.Waambieni wazi wazi kwamba sheria zetu ni hizi na hizi.Sio mpango wa kukataa kurenew kibali cha mtu.Tafsiri ya mambo kama haya huwa sio mazuri hususani katika uundaji wa jumuia changa kama ya Afrika Mashariki.
Nikiangalia matukio kama haya ya kina Waweru na jumuiya ya Afrika Mashariki ndio narudi kule kwenye ukweli kwamba muungano huu utawanufaisha zaidi wakenya na waganda zaidi ya watanzania.Huu ni ukweli kamili.Tusidanganyane.Matukio kama haya ni ushahidi tosha.Watanzania wangapi leo wanafanya kazi Kenya au Uganda ukilinganisha wakenya na waganda wanaofanya kazi Tanzania?
Hivi leo jijini Dar-es-salaam kuna Wakenya chungu mbovu wakichukua ajira ambazo kimsingi zingeweza kabisa kufanywa na watanzania wenyewe.Sasa sababu ni moja au mbili.Kwanza ni elimu na pili ni uzoefu.Angalia jinsi ambavyo wakenya waliopo Tanzani wamejikita katika biashara za mauzo na masoko.Ni kwa sababu wenzetu wamekuwa na vyuo vya taaluma hizo muda mrefu na maendeleo ya viwanda walikuwa mbele ingawa hivi sasa wanaaguka kwa kasi.Wanakuja Tanzania kutumia uzoefu wao.Kiingereza nacho kinawasaidia hivi sasa.Wawekezaji wengi hawataki tena kuwekeza Kenya kutokana na siasa mbovu badala yake wanataka kuwekeza Tanzania.Wanataka watu wanaojua lugha ya kiingereza zaidi.Wakenya wanachangamkia ajira hizi na ndio maana wanazidi kujazana nchini Tanzania.
Kilichotakiwa au kinachotakiwa ni kwa serikali yetu kuangalia kwa undani udhaifu wake na wa wananchi wake kabla ya kuingia tena kwenye jumuia.Ikiwezekana kwa uzoefu mfupi uliojitokeza warudi mezani wakajadili upya jumuia hii.Au la hatua za makusudi zichukuliwe kuwaandaa watanzania kupambana na ushindani huu ndani ya jumuia.Yasipofanyika hayo makubwa zaidi yatatokea mbeleni.
Mimi sina mengi ila ukitizama uchapishaji wa magazeti ya kampuni ya Mwananchi tangu
Waweru aanze kufanya kazi utagundua huyu bwana pamoja na wenzake waliofukuzwa awali ni wajuzi wa uchapishaji.
Nathubutu kusema wameleta mapinduzi ya uandaaji wa magazeti nchini.Printing ni ya hali ya juu, nafikiri wakenya wanao utaalam wa mambo haya kuliko sisi.
Ila kama tunatetea ajira za watanzania mbumbumbu,tuendelee lakini tunajidumaza pale tunapokosa changamoto ya wenzetu.Kampuni ya Nation Media inahitajika sana Tanzania kwani magazeti yaliyopo hakuna kitu cha maana
kinachoandikwa ila ukweli hauwekwi wazi mara nyingi kutokana na woga.
Hili ni pigo kwa maendeleo ya sekta ya habari nchini Tanzania.Ila nahisi kuna mkono wa mtu hapa, kwanini serikali isiwafukuze nchini CEO wengi tu kutoka nchi mbalimbali na inahangaika na wakenya tu?
Serikali inataka kudumaza sekta ya habari ili iendelee na sera za unyanyasaji.
Innocent Kessy
Uganda.
Nadhani tukishabaki na Kasheshe, Komesha, Uwazi na yale mengine ya namna hiyo basi mambo yatakuwa mazuri sana. Nadhani Mwananchi pia litageuka kuwa la udaku au la michezo. Litasaidia sana kutupa habari za fumanizi au uchawi wa Simba na Yanga wakati wa Ligi
Post a Comment
<< Home