8/03/2005

Msomaji Anahoji Kifo cha Garang

Msomaji mmoja (nimemwandikia kumuuliza kama ni sawa nikimtaja jina, kwa sasa sitamtaja), kaniandikia akiuliza maswali kadhaa kufuatia kifo cha Yohana Garang. Ninaweka waraka wake bila kuhariri chochote:

Ndio brother ni siku nyingi hatujawasiliana, umri wangu siyo mkubwa sana ni wakati, na katika kipndi chote hicho nimesha shuhudia (kwa kusikia) vifo vya viongozi wengi na watu wengi maarufu, lakini hakuna kifo kilicho nisikitisha kama cha huyu Mzalendo. Na kwambia bro, huyu ndio Mzalendo wa mwisho katika Afrika aliye baki. Sitaki nizidi kuongea mengi juu yake ilakuna jambo moja nataka unisaidie kufafanua katika makala zako ili na wengine wapate faida,
Bro, nilipo sikia kifo chake, sikuweza kupata usingizi usiku nilikaa na kufikiri usiku kucha,
kwa nini vifo karibu vyote vya viongozi wazalendo wa kiafrika vinahusisha Ajali ya ndege hasa isiyo kuwa na sababu za msingi 'Freak Accident'? ukianzia Samora Michel, Habyarimana na mwenzake yule wa Burundi cypriane Ntayaramira? wakitokea Tanzania kwenye Mkutano,

Samora yeye alitoka kwenye mkutano pia Lusaka, Na huyu tunaambiwa naye alitoka kwenye mkuatano Uganda, Je, hapo kuna kosa mkono wa mtu kweli? Hizo ndege zinazotengenezwa ulaya wanazo tumia Viongozi wetu zina usalama kweli?, najaribu kuwaza kwamba Wazungu walivyo wajanja hawawezi kufunga kamtambo kwenye hiyo ndege wakawa na uwezo wakukikontroli kule kwao wakitaka ianguke wanabonyezatu, Au bro, hii nibiashara maana wazungu walimtumia na kumsaidia sana Savimbi kwa miaka mingi baadae naona walimchoka wakampiga risasi,charlse taylor, Kabila,Osama, Saddam, orodha ni ndefu, sasa wa me amua kumchoka GARANG, naona kunamaslahi fulani wanapata,wakisha mtumia hawataki kuendelea nae tena, walikuwa wanafanya nae siasa sasa wanataka mtu mwingine wa kufanya nae biashara. bro, sorry , kwa barua hii ndefu, naomba ukae ufikirie utanielimisha zaidi katika makala zako, UJUMBE ITABIDI TUBORESHA USAFIRI WETU WA UNGO!!

1 Maoni Yako:

At 8/04/2005 01:59:00 AM, Blogger Indya Nkya said...

Hivi habari hii ya Kifo cha huyu Mwana wa Afrika zimepewa umuhimu gani Tanzania? Hivi kuna salamu za rambirambi zilizotumwa toka serikali ya Tanzania kwa mfano. Nikingalia nukuu za BBC kuhusu kifo cha Garang hadi leo naona ya Museveni na Kibaki, ya kwetu iko wapi?

 

Post a Comment

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com