7/16/2005

Nimekuwa najipumzisha...

Napumzika. Mwili na akili huwa vinahitaji kupumzika. Toka nirudi toka kwenye ule "mchezo wa kuigiza" wa wakuu wa makuhani wa ubepari (mkutano wa genge la wanaume nane, G8) sijaandika chochote hapa. Nimekuwa navuta pumzi, natafakuri, nanyoosha viungo, na kutembea milimani. Nadhani nitarudi rasmi kwenye blogu leo usiku au kesho. Au kesho kutwa. Nausikiliza mwili. Ukisema neno, miye natii. Nawe usiwe unasahau kupumzisha mwili na akili.

5 Maoni Yako:

At 7/19/2005 03:29:00 PM, Anonymous Mumtaz said...

Usijesahau kurudi.

 
At 7/19/2005 03:30:00 PM, Anonymous Rais mtarajiwa said...

Mapumziko hayana mwisho? Una viporo vingi.

 
At 7/20/2005 11:21:00 PM, Blogger msangimdogo said...

Pole sana maana igizo lile bilashaka lilikuwa bab kubwa na lilistahili kuchosha kwa hakika, ni vyema kupumzika kutafakari igizo gani litafuatia baada ya lile.

 
At 7/26/2005 08:16:00 AM, Anonymous Fadhili "mtu wa watu" said...

Dunia yetu hii ni ya maigizo tu. Labda ahera.

 
At 7/30/2005 08:48:00 PM, Anonymous Gatua said...

Ndugu Ndesanjo,
Hujambo! Je si umepumzika ya kutosha sasa?

 

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com