BLOGU YA KISWAHILI KWA AJILI YA KUSAFISHA FIKRA ZA WAAFRIKA!
7/07/2005
SHAMBULIO LA BOMU. AFRIKA, NA G8
Wakati tukijiandaa kuja hapa Gleneagles wanapokutana wakuu wa makuhani wa ubepari,tulipata taarifa za shambulio la kigaidi huko London.Muda mfupi uliopita waziri mkuu wa Uingereza, Tony Balir, ameondoka ghalfa toka kwenye mkutano unaoendelea kwenda London. Tunaambiwa kuwa atarudi. Swali ambalo limekuwa likiulizwa na wengi baada ya shambulio hili ni jinsi ambavyo mkutano huu una hatari ya kupeleka macho kwenye suala la ugaidi zaidi ya suala la Afrika. Mwandishi mmoja kaniambia kuwa viongozi wengi wanapoongea na vyombo vya habari hawazungumzii, kwa mfano, suala la mazingira ambalo liko mezani bali ugaidi. Kwa watu wengi kuna masikitiko kuwa Afrika itawekwa kando na ugaidi kuchukua mstari wa mbele. Mimi binafsi sioni kwanini watu wanasikitika. Nadhani kuna watu wanachukulia kuwa makuhani hawa ni wakombozi wa Afrika wakati ambapo wanachofanya ni kunadi bara letu kwa makampuni yanayomilikiwa na marafiki na jamaa zao. Na makampuni mengi wanamiliki wao wenyewe kwa kupitia hisa. Kuna utani fulani unaendelea hapa. Waandishi wakitaka kwenda kula au bar ambako kila kitu ni bure wanasema, "Ngoja nikafanye umasikini kuwa historia." Wanasema hivi kukejeli kampeni iliyokuwa ikiungwa mkono na serikali ya hapa iitwayo MAKE POVERTY HISTORY.
Mnada wa bara la Afrika ambao umeendelea kwa miaka lukuki na ambao ungehalalishwa rasmi katika kikao hicho unaweza kuahirishwa. Nina maana uhalalishaji wa mnada. Hao wanaume wa Alkaida wanaweza hata kupenya huko Uskochi!!
3 Maoni Yako:

walifikiri kuwa hao jamaa hawawezi kuwafikia huko walipo kwa kifupi Joji kichaka najua kachanganyikiwa hebu tuaambie yuko vipi?
walifikiri kuwa hao jamaa hawawezi kuwafikia huko walipo kwa kifupi Joji kichaka najua kachanganyikiwa hebu tuaambie yuko vipi?
Post a Comment
<< Home