2/06/2005

TOVUTI ZA VYAMA VYA SIASA TANZANIA

Kama kuna jambo zuri lazima pia tuseme. Nimeongea sana juu ya webu za ikulu, bunge, sirikali, ofisi ya waziri mkuu ambazo zina taarifa kwa lugha iliyoazimwa toka kwa malikia Lizabeti. Tovuti ya Chama Cha Mapinduzi (ambayo hayajatokea!) ni mfano mzuri sana. Niliipitia muda kidogo wakati nikiandika tasnifu yangu iliyoitwa Matumizi Ya Zana Teknolojia Mpya Za Habari na Mawasiliano Katika Siasa Tanzania. Toka wakati ule naona imekuwa na mabadiliko makubwa. Imepanuliwa zaidi, ujenzi wake umeimarishwa, rangi imekoa kidogo, na mambo yameongezwa. Ile ya Civic United Front (CUF) naona haina mabadiliko toka nilipoitembelea mara ya mwisho. Zitazame: CCM na CUF.

0 Maoni Yako:

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com