1/23/2005

AMANI TANZANIA NI KIVULI

Mmoja wa wasomaji wangu, Bwana Komba, kaandika maneno mazito sana. Komba simfahamu zaidi ya kupitia mtandaoni. Lakini anayosema yanawakilisha hisia za Watanzania wengi. Nimehariri kidogo sana (sio maudhui bali herufi, vituo, n.k.) waraka wake. Nimeamua kuuweka hapa (bila idhini yake!) kwa watu wote wasome. Nimependa sana pale anapozungumzia kuwa amani Tanzania ni kivuli na kuwa jua likizama...
Huyu hapa Komba:
Nchi za kiafrika bado zinakumbatia watawala hadi sasa, hasa hata nchi yetu Tanzania. Watu wa mbali wanaona kama ni nchi ya Amani kumbe ni nchi ya kibepari inayo wanyanyasa wananchi wake kwani pengo la maskini na tajiri ni kubwa sana. Rushwa ndio mshahara wa viongozi wetu,hakuna kiongozi mwenye huruma na nchi yake,sasa mwisho utafika nasi wanyonge tutachoka na kulala ktk njia kuu ziendazo kwa wakubwa ili haki itendeke kwa wote.

Viongozi wetu ni wafisadi sana na ni waongo sana wakiwa kwenye majukwaa ya siasa utajua ni watu muhimu kumbe wanajifagilia tu ili wale vizuri. Jamani wananchi tuamke na twende kupigania haki zetu hawa waliopo ni makupe tu angalia jinsi wanavyoishi kama wako paradiso,wanajiona wao ndio miungu mtu. Tanzania amani imeisha kimebaki kivuli nacho jua likichwa kitaondoka sijui tutakimbilia wapi? Congo,au Burundi

1 Maoni Yako:

At 8/11/2005 09:34:00 PM, Anonymous Anonymous said...

mambo.

naitwa jon. nataka kusema vipi tu. Na, ninataka kusema ninafikiri watanzania ni watu wapoa, na, siwezi kufikiri ya mahali mbali kuisha ya mapoa na maamani.

ninafikiri kiswahili kwangu ni kibaya sana, sasa; kwasababu, sijamkuja tanzania mpaka 2002. Lakini, ninataka kuja mpale zaidi ya kitu cho chote. Mimi ni Mtanzania kabisa.

Andika tena. Tafadhali.

amani,

jon

 

Post a Comment

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com