6/13/2004

mola tuepushe

Dakika chache zilizopita luninga moja hapa Marekani imeonyesha waandishi walioingia katika eneola jeshi lenye kemikali za sumu. Wameingia katika eneo hilo bila tabu yoyote. Wakaenda hadi kwenye mtambo mkuu wa kemikali na kisha kutoka.
Kisha wakatazama kamera na kuuliza: hivi tungekuwa magaidi?
Eneo hili ni la jeshi. Na eti kuna ulinzi. Mola atuepushe. Nchi hii imekusanya silaha za kemikali, kibaiolojia, na nyuklia. Siku wajamaa hawa wenye madevu wakivamia maeneo hayo…wala sithubutu kufikiria. Tumesikia kuwa kuna magaidi 18,000 ambao usiku na mchana wanafikiria jinsi ya kushambulia Marekani, Wamarekani, na marafiki zao.


1 Maoni Yako:

At 6/13/2004 08:19:00 PM, Blogger shekya said...

Sasa kama unaogopa unafanya nini marekani si urudi kwenu.Tanzania Bongoland kwenye peace na Amani yeuwiiiiiiiiiiiii napamiss sana. Natania Ila kweli kwa nini tuishi kwa wasiwasi.

 

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com