6/13/2004

gongo

Gazeti la The Guardian la Juni 14 linasema kuwa vita dhidi ya pombe ya gongo ni ngumu sana.
Kama Tanzania inashindwa kupambana na biashara ya pombe ya gongo katika jiji la Dar ambako ndio wakuu wa nchi wanaishi, je vita dhidi ya rushwa au umasikini ndio tutaiweza?

1 Maoni Yako:

At 6/13/2004 08:17:00 PM, Blogger shekya said...

Hodi hodi humu ndani.
natumaini kuwa mu wazima nyie.Muheshimiwa Macha, hivi wewe ni mbunge wa jimbo gani sasa hivi?... Na wajumbe mliomo nahoji kuhusiana na swala lililotolewa na mueshimiwa macha kati ya ugumu na uhusiano mbadala uliopo kati ya kutatua tatizo la gongo na umaskini. Macha mimi nafikiri unataarifa sahihi kuhusiana na uuzaji wa gongo au (pombe haramu), Kwa wageni watakaotaka kujua nini maana ya pombe haramu ni pombe ambayo haijadhibitishwa na shirika la viwango yani (TBS) Tanzania Bureau of Standard. Mpo hapo, Kwa mtazamo wangu nasema hivi,uuzaji wa gongo na mazingira ya soko ndio yanayofanya serikali ishindwe kupigana na vita hii. Fikiria zile nyumba za vingunguti,mbagala,mwananyamala. Jiweke katka hali ya kazi naumtathmini askali anayelipwa shilingi 45,000 kwa mwezi. Na sio kwa mwezi kwamba unapata hiyo hela , huo mwezi ni msululu kuna vikwazo vya hapa na pale vinavyosababisha kupata pesa baada ya muda mrefu.wewe askari ujala toka ahsubuhi,mtoto nyumbani naumwa, hunauhakika wa kazi, familia inakulilia njaa,watoto wanataka ada ya shule,mwenye nyumba anataka kodi? Hebu vuta pumzi kwanza jiulize tutafika. Hakuna askari atakayefanya kazi katika mzingira kama haya asipikee rushwa ni uongo hasa kwa nchimaskini kama Tanzania. Serikali kupigana na vita ya gongo wapiganaji lazima wapewe siraha( mshahara mzuri,chakula,mavazi,maradhi,afya,n.k). Zaidi ya hayo wanaanchi pia hawajapata elimu ya kutosha au elimu haija wafikia walengwa. Hebu fikiria maendeleo ya sayansi na teknologia, ni nani anyeyapata hayo kwa nchi kama Tanzania. Wanunuzi wa gongo hawana redio, Televisheni(runinga) wala hawanunui magazeti watajulia wapi kwamba gongo ina madhara mwilini mwao.

Macha kutokana na hayo machache nafikiri serikali ya tanzania haijashindwa kupigana na hii vita kwa kuwa inapenda kushindwa ila tu ni kwamba haiwezi hata kama itajiribu kutokana na hiyo hali niliyoeleza hapo juu. Kama hali itabadilika srikali inaweza kupigana na swala la gongo. Na kwa kumalizia, Hebu piga picha ya ramani ya majengo katika nchi zilizoendelea, Hivi macha kweli wewe serikali itaweza kumfikia kila muuzaji wa pombe haramu. Ingekuwa marekani ningesema sawa.Kila nyumba inajulikana iko wapi. Tanzania nyumba haziko katika mstaali myoofu, zimepinda gata askali ataogopa kuingia ndani na kuatarisha maisha(kuuwawa). Sijui umenipata hapo.


Tukirudi katika swala la kupigana na umaskini. Nadhani inawezekena kwa sasa.Na ningependa kukumbushia pia ukilinganisha upiganaji wa gongo na umaskini nafikiri upiganaji wa umaskini unaweza kuwa nafuu na wenye kuzaa matunda zaidi ya upigani wa gongo.

Swala la upiganaji wa umaskini linawezekana kwa tanzania. Mfano mzuri tumeuona juzi wakati Muheshimiwa Mramba alipowakilisha bajeti bungeni, Uchumi wa nchi unakua, Utegemegezi unapungua, na swala la maendeleo ya jamii wafadhili wamechangia kwa kadri ya uwezo na mapato ya nchi yaongezeka. Kama unayoolewa ukiwa mtaalamu wa mahesabu wewe ni kutoa numba tu uchumi utaongezeka kwa asilia kadhaaa kama wanannchi wameelewa au hawajaelewa shauri yao wewe kama mbunge umetimiza wajibu , sijui unanipata. Sasa hivi tanzania kuna ongezeko la matumizi ya komputer, kuna cash machine, barabara nzuri, plaza, supermarketi nzuri sana za kukutoa ushamba, wananchi wana maji safi, visima, hospitali zahanati, elimu ya shule ya msingi ni bure na lazima .Mzazi usipompeleka mtoto shule mahakamani unaona hapo, angalau kamsukumo kapo.

nafikiri ningeongea mengi tena kwa uchambuzi safi kabisa maana mimi ni mwana jamii lakini sijajua wasomaji wantaka nini na kipi kitawabore .Mana mpaka hapa nahisi nimeongea mengi mno, watu watashindwa kusoma au kuboreka . Lakini kwa kumalizia vita dhidi ya umasiki inawezekana ukilinganisha na gongo. Labda na weza kuandika zaidi endapo utanipa nafasi na wanabodi wako tayari kusoma nakala ndefu.

Tatizo ni moja tu litakalo bakia Ukimwi. Kama watanzania tuanakufa kama samaki hatuwezi kupigana na hii vita. Wasomi watakufa, viongozi watakufa, wazazi watakufa,wataalamu watakufa,wanasheria,madaktari watakufa,n.k. watu wote wenye nafasi nzuri za kuchangia maarifa katika upiganaji wa umaskini watakufa.Mwisho ukoloniiiiiiii huooooooooooo unapiga hodi ............Jamani watanzania tujipendeeeeeeeeeee.......


ahsanteniiiiiiiiiii

 

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com