6/13/2004

ndizi

Kesho lazima nile ndizi za kukaanga. Ndizi "Uganda" toka Karibiani. Hawa jamaa sijui wanapendea nini vyakula vyao. Vyakula vimejaa kemikali utafikiri watu wana wadudu wa kahawa mwilini mwao wanataka kuwaua!

Nimemaliza kutazama mkanda wa video wa Louis Farrakhan. Huyu ni kiongozi wa Taifa la Waislamu (Nation of Islam). Kundi la watu weusi wanaoamini kuwa uislamu ni dini ya Waafrika na kuwa nabii Eliya aliyetabiriwa kwenye biblia ni mwamerika mweusi aitwaye Elijah Muhammad, ambaye ndiye aliyejenga kundi hili. Wanaamini kuwa Elijah alikutana na mtu aitwaye Farad Muhammad ambaye alimfundisha Elijah Ukweli juu ya dunia, mungu, na wanadamu kwa miaka mitatu. Baada ya miaka mitatu Farad alitokomea.

Basi Farrakhan ni mzungumzaji hodari sana. Ana kipaji cha kuongea.

Makala yangu kwenye Mwananchi wiki mbili sasa imekuwa ikizungumzia juu ya Urasta. Nitamalizia wiki ijayo kisha nitaandika juu ya Taifa la Waislamu.

Naenda kupumzika.

2 Maoni Yako:

At 7/21/2004 01:19:00 PM, Anonymous Anonymous said...

From Critic,

Kwanza kabisa pongezi sana kwa blog yako (sijui Kiswahili inaitwaje, niwie radhi) inayonifanya kuona kuwa bado kuna matumaini kwa angalau mawazo ya kimapinduzi kukutana na kujengana.


Louis Farakhan ni msemaji mzuri, lakini hata Hitler naye alikuwa msemaji mzuri vile vile.

Sikatai kuwa Taifa la Waislamu lina maswala mengi tu muhimu, lakini kwa kusoma "The Autobiography of Malcom X" nimegundua kuwa mapinduzi ni magumu sana.Mimi sijafika kwenye msikiti wao wa hapa New York lakini siwezi kushangaa kama kuna mapotosho ya uislamu orthodox ili kufikia lengo la kisiasa.

Kama wanataka chombo cha kisiasa waweke wazi nia yao.Kama wanataka dini inayoangalia Afrika zaidi hata uislamu siyo hiyo dini, kwa maana kulikuwa na dini kibao Afrika kabla uislamu kuingia.

 
At 8/01/2004 01:50:00 PM, Anonymous Anonymous said...

From Critic,

Ndesa wiii!

anuanipepe yangu ni jiggah75@hotmail.com, tuna mengi sana ya kuzungumza.

 

Post a Comment

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com