6/13/2004

UJUMBE WA LEO

Ujumbe wa Leo: Kila ujualo ni uongo.
************************************

Umekuwa ukidanganywa toka uzaliwe. Mababu zako walidanganywa. Wazazi wako walidanganywa. Wewe nawe umedanganywa. Wanao utawadanganya. Basi dunia nzima imejaa uongo mtupu.

1 Maoni Yako:

At 8/01/2004 02:06:00 PM, Anonymous Anonymous said...

From Critic,

Ndesa,

Msingi wa uchambuzi wako kwamba kila ujualo ni uongo unaanguka pale unapoanza kuuchambua huo huo msingi wenyewe.Kama unajua kuwa kila ujualo ni uongo, na kama unalitumia neno kila kwa maana ya kila na siyo kwa "effect" ya uandishi, basi hata huo msingi unaoutumia pia ni uongo.Ukiuhasi msemo wako "kila ulijualo ni uongo" unaenda kwenye mwisho mwingine wa upinde huu unaokuletea utambuzi kuwa kila ulijualo ni kweli.Hii ndiyo kusema, kama kila ulijualo ni uongo, hata usipoenda mbali na kuanza kuuchambua huo usemi unarudi kwenye negation yake kwamba kila ulijualo ni ukweli.Natumaini ulikuwa unaandika kwa effect na siyo literally.

Lakini kujua ni nini?Kujua ni sawa na kuamini? Kama ni sawa kwa nini? Kama si sawa, wapi unajua na wapi unaamini? Maana katika mwanzo mmoja wa upinde huu muamini sana huamini kila kitu, huamini mungu kaumba dunia na mbingu katika siku sita na kupumzika ya saba, huamini serikali itamsaidia akizeeka,huamini kuwa shetani ndiyo mwanzo wa matatizo, na ujinga mwingine mwingi tu kama huo.

Katika upande mwingine wa shilingi hiyo hiyo kuna mwanafalsafa anayehoji uwepo wa mungu kwa kuuliza kama universe ilianza kwa bing bang au iliumbwa? Creation au evolution, mwanafalsafa huyu huweza hata kufikia kuhoji uwepo wake mwenyewe kwamba hivi ni kweli tunaishi au ni ndoto moja kubwa tu ambayo ina kila kitu tunachokiona kugusa kunusa na kuonja na sisi tunafikiri kwamba tunaishi.

Mimi ninajua kuna sehemu hapo katikati ndiyo inaelezea hali halisi vizuri zaidi.

 

Post a Comment

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com